France Football kwa mwaka 2018 imetaja list ya mastaa wa soka wanaoongoza kuingiza pesa nyingi kwa mwaka 2018 huku Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa FC Barcelona wamebadilishana nafasi ya kwanza baada ya Ronaldo kuongoza mwaka uliyopita.
List hii imepangwa kwa kuzingatia malipo ya mishahara ya wiki ya wachezaji, bonansi za mechi na mapato ya mikataba binafsi ya matangazo, kitu ambacho kimesaidia sana kwa kiwango, hii ndio TOP 10 yenyewe mtu wangu.
10- Luis Suarez yeye ametajwa katika nafasi ya 10 akiingiza pound milioni 22.7 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 70, pia Suarez amefanikiwa kuwa moja kati ya nguzo muhimu za ufungaji katika kikosi cha Barcelona.
9- Mshambuliaji wa Atletico Madrid ya Hispania Antoine Griezmann kwa kuingiza zaidi ya pound milioni 22.7 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 70, akimzidi Luis Suarez kwa point chache lakini ndio mchezaji pekee wa Atletico aliyefanikiwa kuingia katika list hii.
8- Pamoja na kuwa Zlatan Ibrahimovic hakuwa na mwanzo mzuri wa msimu akiwa na Man United kutokana na kuwa na majeruhi na sasa amejiunga na LA Galaxy ya Marekani Zlatan anaingiza pound milioni 23.4 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 74.
7- Beki wa Real Madrid na nahodha wa timu hiyo Sergio Ramos yeye yupo nafasi ya 7 akiingiza kiasi cha pound milioni 24.1 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 76 akizidiwa na beki mmoja tu ambaye ni Gerard Pique wa Barcelona lakini wanacheza nae timu mmoja ya taifa.
6- Staa wa Real Madrid Toni Kroos ndio mchezaji pekee wa taifa la Ujerumani anayeingiza pesa nyingi kwa mwaka na katika list hii akiwa nafasi ya 6 kwa wachezaji wanaoingiza pesa nyingi duniani kwa mwaka akiingiza pound milioni 24.7 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 78.
5-Beki pekee duniani aliyeingiza pesa nyingi kwa mwaka ni Gerard Pique wa timu ya taifa ya Hispania na club ya FC Barcelona ya Hispania, Pique katika list hii ametajwa namba 5 kwa kuingiza kiasi cha pound milioni 25.4 ambazo ni zaidi Tsh bilioni 80.
4- Nafasi ya nne inakwenda kwa Gareth Bale wa Real Madrid ambaye kwa mwaka yeye anatajwa kuingiza kiasi cha pound milioni 38.5 ambacho ni zaidi ya Tsh Bilioni 120 licha ya kuwa kwa sasa soka lake limekuwa likikumbana na mitihani mingi kwa sababu ya kupata majeruhi mara kwa mara.
3- Neymar yupo nafasi ya tatu akiingiza kiasi cha pound milioni 71.3 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 225, lakini akitajwa kama ndio mchezaji ghali zaidi duniani baada ya kuondoka Barcelona nakujiunga na Paris Saint Germain ya Ufaransa kwa ada ya dunia.
2- Cristiano Ronaldo baada ya kuwa kinara kwa mwaka uliyopita mwaka huu ameshika nafasi ya pili kwa kuingiza kiasi cha pound milioni 82.2 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 260 kwa mwaka, akizidiwa na Lionel Messi ambaye mwaka uliyopita alikuwa nafasi ya pili.
1- Lionel Messi kwa mwaka huu ameongoza kwa kuingiza kiasi cha pound milioni 110 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 340, yeye ndio mchezaji anayevuna pesa nyingi kwa mwaka kuliko mchezaji yoyote duniani.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao