Taasisi ya Tiba ya Mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) imefanikisha kumfanyia upasuaji wa kichwa mgonjwa aliyekuwa akisumbuliwa na uvimbe ndani ya ubongo uliomsababishia kupoteza uwezo wa kuona katika macho yote mawili.
Akiongea ndani ya Chumba cha Upasuaji Dr. Laurent Mchome ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo amesema mgonjwa huyo alikuwa na uvimbe aliokaa nao kwa miaka mitano.
“Mgonjwa huyu ana uvimbe ambao amekaa nao kwa muda miaka 5, alianza kwa kupoteza uwezo wa kuona, baada ya kufanya vipimo vingi hawakujua tatizo ni kitu gani, tumefungua upande wa kulia wa kichwa, ili tuweze kutoa vitu vilivyo ndani ya uvimbe,” – Dr. Laurent Mchome
MIAKA 11 ILIYOPITA: WALICHANGIA UJENZI WA ZAHANATI LAKINI HAIJAFUNGULIWA HADI LEO, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA