Mwanzoni mwa mwaka 2016 Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali, Msichana Initiative linalotetea haki za wasichana kupata elimu, Rebeca Gyumi alifungua shauri mahakamani kupinga kifungu cha 13 na 17 cha sheria ya ndoa kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.
Maamuzi ya mahakama ni kwamba serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu kujipanga ili kuvirekebisha vipengele hivi tata ndani ya mwaka mmoja.
Kwenye interview hii na Ayo TV , Rebeca Gyumi ameelezea mpango wao baada ya kushinda kesi hiyo……>>>’tuna mpango wa kukaa na kuangalia ni kwa jinsi gani tunaweza kuwahusisha wadau wote muhimu ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii, kwa sababu ni muhimu sana kwa jamii kuweza kuelewa athari ya ndoa za utotoni’.
ULIKOSA MAWILI YA MTAALAM WA SAIKOLOJIA CHRIS MAUKI KUHUU USHOGA? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI