Baada ya Simba kupoteza point mbili Shinyanga kwa kutoka sare dhidi ya Mwadui FC, leo walionekana kufuta makosa na kuifunga Mbao FC magoli 5-0, magoli ya Simba yakofunhwa ma Shiza Kichuya dakika ya 38, Okwi aliyefunga mawili dakika ya 41 kwa penati na 68, Erasto Nyoni dakika ya 82 na Nikolaos Gyan dakika ya 86.
Game imemalizika kwa Okwi kuweka rekodi baada ya kufunga magoli mawili leo na kufikisha jumla ya magoli 16 akicheza game 15 VPL msimu huu, akivunja rekodi ya Abdurahman Musa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva waliobuka wafungaji bora msimu uliyopita kwa kufunga jumla ya magoli 14 kila mmoja, hivyo Okwi kavunja rekodi hiyo akicheza game chache.
Kabla ya Simba kupata goli hata moja benchi la ufundi la Simba lilifanya mabadiliko mapema kabisa kipindi cha kwanza kwa kumtoa Said Hamisi Ndemla na kumuingiza Mzamiru Yassin mabadiliko ambayo yalizaa matunda.
Baada ya Ndemla kutolewa inadaiwa kuwa hakutaka kumpa mkono kocha wake msaidIzi Masoud Djuma, hivyo baada ya game tulimuuliza Maoud Djuma kuhusiana na kitendo hicho.
“Hata mwanamke nyumbani kuna siku mnashindwa kusalimiana na kupeana mkono, hakupi hata kiss hiyo ni mambo ya kawaida kupewa mkono sio lazima lakini kama mchezaji game imemkataa tunamtoa tuna muweka mwingine”>>> Masoud Djuma
VIDEO: Simba hii haikamatiki vs Mbao FC, Full Time 5-0