Watanzania wanne wenye vipaji wamefanikiwa kupata nafasi ya kwenda Nairobi Kenya kwenda kusoma masuala ya filamu katika kipindi cha mwaka mmoja, watanzania hao wanne ni miongoni mwa vijana 60 kutoka nchi mbalimbali Afrika waliopata nafasi ya kushinda nafasi hiyo.
Washindi hao wanne wamepatikana kutokana na shindano la Multchoice Talent Factory lililoendeshwa na kampuni ya Multichoice Tanzania, hivyo washindi wote wanne watatakiwa kuripoti Nairobi October 1 2018 ili kuanza mafunzo hayo katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mchakato mzima wa kuwapata washindi hao ulianza May 20 2018, ambapo kwa Tanzania ni zaidi ya watu 160 ndio walikuwa wametuma maombi na hatimae kupatikana washindi wanne pekee baada ya July 20 kufanyika kwa mchujo huo.
Rais Magufuli atoa kauli makontena ya Makonda