Baada ya mchezo dhidi ya USM Alger kuonekana kwa mwenyekiti wa Yanga Yussuf Manji kama amekubali kurejea na kuungana na timu hiyo, baada ya kuomba kwa muda mrefu maswali yalikuwa mengi kama Manji amerudi rasmi Yanga au kaenda kuihamasisha timu ishinde kama shabiki wa kawaida wa Yanga.
Baada ya stori hizo kuenea Ayo TV ilimtafuta aliyekuwa katibu wa baraza la wazee wa Yanga mzee Ibrahim Akilimali ambaye amekubali kuzungumzia ishu ya kurudi kwa Manji ndani ya Yanga “Hili ndio kama sisi tumerogwa nalo haya twendeni hivyo hivyo, tunasema kuwa mwenyekiti wetu tulikuwa tunampenda japo watu wanatuchonganisha, yeye ndio kaamua kujiuzulu, sasa wanaosema karudi mwenyewe mbona hasemi wanamsemea”
Kocha amewaondoa wachezaji wa Simba, katika kikosi cha Taifa Stars