Kampuni ya Star Media na SOS Children’s Villages Tanzania wametia saini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi, lengo likiwa ni kuwapatia fursa mbalimbali hasa kiteknologia ili kuendana na malengo ya Milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Katika mkataba huo StarTimes itakuwa ikisaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika mikoa zaidi ya saba (Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi) hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village.
Moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni kuwapatia nafasi Vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.
Pia kampuni ya Star Media (T) Ltd itatumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuzungumzia juu ya programu za SOS Village ikiwa ni moja ya mambo ambayo yatafanywa chini ya ushirikiano huo ambao ni nafasi ya kipekee kwa Vijana kukua.
Ushirikiano na StarTimes unawakilisha jinsi ambavyo SOS Village inapiga hatua katika kuwapeleka Vijana katika soko la ajira na kuwapatia namna ama njia za kujitengenezea kesho yenye uimara na uhakika zaidi katika jamii zao.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19