Baada ya Tanzania kukosa wawakilishi wa michuano ya Afrika katika hatua ya Makundi msimu uliyomalizika, hatimae leo Club ya Yanga imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa kuitoa Waloitta Dicha ya Ethiopia katika hatua ya mtoano.
Yanga leo wakiwa mjini Awassa Ethiopia katika mchezo wa marudiano wamepoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Esheti Mena dakika ya 2 ila wanafanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla ya agg ya 2-1, hiyo ni baada ya mchezo wa kwanza Yanga kupata ushindi wa magoli 2-0 uwanja wa Taifa.
Baada ya matokeo hayo Yanga wanafuzu hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili, mara ya mwisho Yanga kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo ilikuwa 2016, ambapo walipangwa na MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Congo DRC na Medeama ya Ghana.
Yanga wamerudia rekodi yao ya mwaka 2016 ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo na waliingia hatua ya Makundi mwaka huo kwa kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1 licha ya mchezo wa marudiano kufungwa goli 1-0.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI