Moja kati ya stori zilizochukua headlines katika soka bongo ni pamoja na maamuzi ya benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kutangaza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kilichokuwa na majina ya wachezaji 24 huku likiwemo jina la Thomas Ulimwengu.
Mjadala umezuka kufuatia Ulimwengu kudaiwa kuwa alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza jeraha la goti, sasa kitendo cha kuitwa wengi walitaka kujua ni kwa kufuata kanuni gani hadi wamefikia maamuzi ya kumuita Taifa Stars.
Beki wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa Afrika Kusini katika club ya Baroka FC Abdi Banda ambaye nae ni sehemu ya kikosi hicho, amedaiwa kama kusikitishwa na watu wanaokosoa kuitwa kwa Ulimwengu na kufikia kuandika ujumbe huu “Waliomuua GADDAF ni watu wa LIBYA wenyewe sio nchi jiran. @thomasulimwengu From ZERO to HERO”
VIDEO: Kocha kajibu kuhusu kumuita Thomas Ulimwengu Taifa Stars