Staa wa soka wa zamani wa vilabu vya Man United, Real Madrid, AC Milan na LA Galaxy ya Marekani David Beckham amekiri hadharani kuwa ndoa yake na mkewe Victoria Beckham iliyodumu kwa miaka 19 ni ngumu.
Beckham amekiri kwa mafumbo kuwa ndoa yake ni ngumu, kitu ambacho kimeanza kuhusishwa na kauli ya Victoria Beckham aliyoitoa kwa watoto wake, wiki kadhaa nyuma Victoria Beckham aliripotiwa kuwa aliwaambia watoto wao wanne kuwa baba yao amekuwa na tabia za kisaliti katika ndoa.
Staa huyo wa soka amenukuliwa na kituo cha TV cha Australia kupitia kipindi cha The Sunday Project “Ndoa yangu imekuwa kidogo ngumu”
Ndoa ya David Beckham na Victoria Beckham imedumu kwa miaka 19 sasa lakini inaonekana inapitia kipindi kigumu kwa sasa, Beckham na Victoria wamefanikiwa kupata watoto wanne Blooklyn, Romeo, Cruz na mtoto pekee wa kike Harper Seven.
Samatta alivyofutwa miguu baada ya game