Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliozikutanisha Simba ya Tanzania na Al Masry ya Misri uliochezwa Jumatano March 7 2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam umeingiza jumla ya shilingi Milioni 85,045,000.
Mchezo wa Simba dhidi ya Al Masry uliingiza jumla ya mashabiki 14,798 , VIP A waliingia Watazamaji 250 kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000,VIP B na C waliingia, Watazamaji 557 kwa kiingilio cha shilingi 15,000 ikapatikana jumla ya shilingi 8,355,000.
Majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 13,644 kwa kiingilio ncha shilingi 5,000 imepatikana jumla ya shilingi 68,220,000
Mgawanyo wa mapato
VAT 12,972,966.10
Selcom 5,017,655.00
TFF 3,352,718.94
Uwanja 10,058,156.83
Simba 43,585,346.28
Gharama za mchezo 6,034,894.10
BMT 670,543.79
CAF 3,352,718.94
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry