Ligi Kuu ya Ugiriki leo Jumatatu ya March 12 2018 imetangazwa kusimamishwa kwa muda usiojulikana kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wa PAOK dhidi ya AEK Athens uliyochezwa Jumapili ya March 11 2018.
Sababu kubwa iliyofanya Ligi hiyo kusimama ni kutokana na Rais wa club ya PAOK Ivan Savvidis kuingia uwanjani na bastola wakati wa mchezo wa PAOK dhidi ya AEK Athens na kupelekea game hiyo kuahiriashwa.
Baada ya tukio hilo waziri wa michezo wa Ugiriki Giorgos Vasileiadis baada ya kukaa na kukutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Alexis Tsipras leo Jumatatu ya March 12 wametangaza kuisimamisha Ligi hiyo kwa muda usiojulikana.
Savvidis ambaye ni mmiliki wa club ya PAOK aliingia uwanjani kupinga maamuzi ya refa Giorgios Kominis kulikataa goli la timu yake lililofungwa na dakika ya 90 ikisemekana kuwa ni offside lakini mchezo uliahirishwa masaa mawili baadae baada ya wachezaji wa AEK kugoma kurudi uwanjani.
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry