Jumatano ya March 28 2018 African Banking Summit iliandaa mkutano maalum uliyopewa jina la African Insuarence Summit katika ukumbi wa Mlimani City na kuzikutanisha kampuni mbalimbali za Bima pamoja na kamishina mkuu wa mamlaka ya Bima aliyewakilishwa na Elia Kajiba.
African Insuarence Summit uliyofanyika leo na kuhudhuriwa na mkurugenzi wa ufuatiliaji Elia Kajiba pamoja na kuwakutanisha wadau wa Bima na makampuni ya Bima ulikuwa na ugeni kutoka nchi nne za Afrika ambazo ni Rwanda, Kenya, Afrika Kusini na Nigeria.
Kuelekea kuzindua mkutano huo Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa wa mamlaka ya Bima Elia Kajiba alilazimika kujibu maswali kadhaa ya waandishi wa habari kuhusiana na kampuni feki za Bima na ucheleweshwaji wa malipo kwa wateja wa Bima ambao wanakuwa wamekatia Bima kubwa mali zao na zimepata matatizo.
“Kama wadau wa Bima tunawajibu wa kuelimisha jamii tuko hapa kwa sababu ni mahali ambapo wanakuja watu wengi, kama mamlaka jukumu letu kubwa kabisa tulilokuwa nalo ni kuyasajili makampuni ya BIMA, sheria inasema hakuna kampuni yoyote inayoweza kufanya shughuli za BIMA kama haijasajiliwa”>>> Elia Kajiba
“Sasa kama kuna kitu kinaitwa feki wewe mwananchi ni vizuri ukatuletea taarifa ili tuweze kuzifanyia kazi lakini kama tutamkuta mtu anafanya shughuli za BIMA bila kusajiliwa adhabu zake ni kubwa ni faini ya Tsh milioni 5 pamoja na kifungo cha miaka miwili jela”>>> Elia Kajiba
Ayo TV MAGAZETI: Viongozi wa CAHDEMA wamelala Segerea, JPM alivyoandika barua 25 kwa JK