Uongozi wa club ya Ruvu Shooting leo February 6 2018 wametangaza kufikia maamuzi ya kumuomba msamaha mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayeichezea Simba SC ya Tanzania Emmanuel Okwi kutokana na tukio lililomtokea.
Ruvu Shooting wametangaza kumuomba msamaha Emmanuel Okwi na club yake ya Simba kufuatia kitendo alichofanyiwa Okwi na mchezaji wa Ruvu Shootig Mau Bofu wakati wa mchezo dhidi yao, Mau Bofu alimpiga kiwiko cha makusudi Okwi na kumfanya apoteze fahamu.
Okwi alishindwa kuendelea na mchezo dakika ya 46 kipindi cha kwanza, baada ya kupigwa kiwiko na kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa magoli 3-0.
Tazama video yenyewe hapa chini kwa kubonyeza PLAY