Staa wa timu ya taifa ya England anayeichezea Tottenham Hotspurs Harry Kane Jumapili iliyopita katika ushindi wa 4-1 wa timu yake dhidi ya Bournemouth Ligi Kuu England alishindwa kumaliza game kwa kupata majeraha, kitu ambacho kimeongeza hofu kwa anaweza kukosa Kombe la dunia.
Baada ya hofu hiyo kuwa Harry Kane anaweza akawa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, kitu ambacho kilileta hofu timu ya taifa ya England kama wanaweza kumpata nyota huyo katika fainali za kombe la dunia 2018 zitakazofanyika Urusi.
Hata hivyo baada ya kufanyiwa vipimo na kufanyiwa scan imegundulikwa kuwa jeraha lake la mguu wa kulia la Harry Kane litamuweka nje ya uwanja hadi mwezi ujao, hivyo katika fainali za Kombe la dunia atakuwa na nafasi ya kuitumikia England kama kawaida ingawa ataukosa michezo ya kirafiki ya England dhidi ya Uholanzi na Italy.
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry