Imekuwa ni kawaida kwa watanzania au wasanii wa kitanzani wengi kuwa na tamaduni za kwenda nje ya nchi na ma-director na wapiga picha wao ku-shoot video zao za muziki, lengo lao likiwa kwenda nje kutumia location za huko ila wanakuwa wametoka na watu wao.
Mtanzania na msanii chipukizi wa nyimbo za Injili Modest Kuhani anayefanya kazi na kuishi nchini Marekani ameeleza ilivyokuwa changamoto kupata maeneo ya kufanya music video, changamoto kubwa iliyopo ni kuwa wapiga picha za video Marekani ni lazima wawe na vitambulisho maalum hivyo kama una director wako wa video ndio unaenda nae unaweza usipate nafasi ya kushuti.
Modest ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa Injili wa ‘Hatujafika’ kwa sasa, akifanya mahojiano na AyoTV kwa njia ya simu ameeleza dhamira yake ya kutaka kurudi Tanzania 2020 kufanya muziki wake hapa lakini amewataja na wanamuziki wa nyimbo za Injili anaotamani kufanya nao kazi.Bonyeza PLAY kusikiliza interview yenyewe.
VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati