Michuano ya UEFA Europa League inaendelea tena usiku wa November 29 2018 kwa michezo mbalimbali kuchezwa, baadhi ya timu tayari zimejithibitishia nafasi ya kuingia hatua ya mtoano kutokana na kuvuna point mapema katika michezo ya awali.
Wawakilishi pekee wa Ligi ya England Chelsea na Arsenal wao tayari wameshajihakikishia kufuzu, lakini AC Milan na Celtic bado hali ni tete, huku mabingwa wa zamani wa Ulaya Olympique Marseille wameshayaaga mashindano hayo kutokana na kukosa point za kutosha.
Arsenal wanahitaji ushindi nchini Ukraine watakapocheza dhidi ya Vorskla Poltava ili waweze kuongoza Kundi E huku wakifuatiwa na Sporting Lisbon bila kujali matokeo ya michezo ya mwisho wiki mbili zijazo.
Kocha wa Arsenal Unai Emery anatarajia kuwapumzisha baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza katika mchezo huo, huku mshambuliaji mwenye kiwango bora kabisa Pierre Emerick Aubameyang akitarajiwa kukaa nje pia ili kupumzusha, michezo hii yote inaonyeshwa moja kwa moja na chaneli za michezo katika king’amuzi cha StarTimes.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?
https://youtu.be/RSeYrwNEO9M