Baada ya usiku wa April 3 kufahamu kuwa timu za Real Madrid na Liverpool ndio zitacheza fainali ya UEFA Champions League May 26 mjini Kyiv, usiku wa May 3 pia tumezifahamu timu zitakazocheza fainali ya UEFA Europa League baada ya michezo ya marudiano ya nusu fainali kuchezwa.
Club ya Arsenal ambayo ikuwa ugenini kucheza dhidi ya Atletico Madrid baada ya mchezo wa kwanza katika uwanja wao wa Emirates kumalizika kwa sare ya 1-1, wamejikuta wakiondolewa katika michuano hiyo kwa kipigo cha goli 1-0 lililofungwa na Diego Costa dakika ya 45 ya mchezo.
Kwa matokeo hayo Arsenal wanatolewa katika michuano ya Europa League kwa Aggregate ya magoli 2-1 dhidi ya Atletico, sasa game ya fainali itachezwa May 16 Lyon Ufaransa kati ya Atleico Madrid dhidi ya Marseille iliyoitoa Salzburg kwa aggregate ya magoli 3-2 baada ya game ya leo kumalizika kwa Marseille kupoteza kwa magoli 2-1 ugenini.
Kwa maana hiyo baada ya Arsenal kutolewa leo katika nusu fainali ya michuano ya Europa League, kocha wao Arsene Wenger anayeondoka mwisho wa msimu huu katika miaka yake 22 aliyowahi kuifundisha Arsenal anaondoka pasipo kutwaa taji lolote Ulaya.
VIDEO: Mbwembwe za Haji Manara uwanjani baada ya ushindi wa Simba vs Yanga