Zikiwa zimesalia siku chache kumalizika kwa vikao vya bunge la 11 linaloendelea Dodoma, bado wabunge wameendelea kuwasilisha michango yao. Leo nakusogeza karibu na mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye kaamua kuikumbusha serikali kufanya marekebisho ya sheria inayohusu mahakama ya mafisadi ambapo inaonyesha wahusika watakuwa ni wale wa kuanzia tuhuma za bilioni moja.
Bashe anasema…>>>’Uanzishwaji wa division ya mahakama ya mafisadi inaonyesha dhamira njema ya serikali katika kupambana na rushwa, lakini nataka kushauri kiwango cha shilingi bilioni 1 ni kikubwa sana. Ningeshauri serikali ukangalia uwezekano wa kubadilisha kiwango hicho‘ –Hussein Bashe
‘Ni walau iwe kutoka milioni 100, nasema hivi kwasababu tutaenda kujaza kesi katika mahakama zingine za uhujumu uchumi na dhana nzima ya kupambana na rushwa itakuwa imekosa nguvu na hii wataalamu wa kula rushwa watakuwa wajanja na kuhakikisha rushwa zao hazifiki huko‘ –Hussein Bashe
Unaweza kuendelea kumsikiliza mbunge Hussein Bashe kwenye hii video hapa chini…
ULIIMISS HII YA MBUNGE HUSSEIN BASHE KUSEMA ‘KAMA MNATUKATA KODI MKATENI NA RAIS’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE