Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi na Makazi John Lupalo amekutana na wadau wa Ardhi na Makazi kujadili changamoto za kuweza kuwasilisha katika Mkutano Mkuu wa Mipango Miji duniani utakaofanyika mwezi February 2018 nchini Malaysia.
Ameeleza kuwa kama nchi itafanikiwa kwa miaka 10 ijayo kuhakikisha kila kipande cha ardhi kimetambuliwa, kupimwa na kumilikishwa, wananchi wataweza kutumia maeneo yao ya ardhi kama mtaji.
“Tukiweza kupanga, kupima na kumilikisha ardhi vizuri, itakuwa fursa kubwa sana kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kukopa, kuongeza thamani ya ardhi yao, hii itawasaidia wananchi hata wale wasio na ajira rasmi.” – John Lupalo
BREAKING ‘Ninawapa wiki moja la sivyo tutavunja mkataba na TBA’- Waziri Ndalichako
Kifo cha Mama aliyegonga Ndege Airport Mwanza