Mchakato wa kuanzisha umoja wa fedha unaolenga kuanzishwa kwa sarafu moja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulianza januari 2011 wakati majadiliano kati ya nchi wanachama wa jumuiya wa Afrika Mashariki kuandaa itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha yalipoanza rasmi.
Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Lusajo Mwankemwa ametuelezea vitu hivi ambavyo unatakiwa kuvifahamu pale tutakapoanza kutumia sarafu moja ya Afrika Mashariki. zipo faida itakayopata Tanzania kutokana na umoja wa fedha na hasa kuwepo kwa sarafu moja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni pamoja na……….
Kupunguza gharama za kufanya biashara katika Nchi wanachama na hivyo kuhamasisha ukuaji wa biashara baina ya nchi wanachama na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
Kwa kuwa na sarafu moja, umoja wa fedha utaepusha athari za ubadilishaji wa fedha ndani ya jumuiya.
Kuwezesha nchi wanachama kuwa na kiwango kidogo na tulivu cha mfumuko wa bei (low and stable inflation).
Kuwezesha nchi wanachama kuwa na viwango vidogo vya riba vya kukopa (low interest rates).
Kutumia sarafu moja kutaleta uwazi katika bei na hivyo kuongeza ushindani wa soko ndani ya Jumuiya.