March 1 2016 kwenye Hekaheka ya Clouds FM, Geah Habib ametuletea hekaheka iliyotokea Magomeni Dar es salaam hii ni baada ya Mtoto kupigwa na Mama anayeishi naye, tukio ambalo limepelekea mpaka majirani na mjumbe wa eneo hilo kuingilia kati.
‘Naitwa Pilli Mdidi mjumbe wa shina namba 12 nakaa mtaa wa Kiembeni nilivyopata taarifa nimeacha kupika, maana mimi ni Mama Lishe ndio nimefika hapa ndio nikaadisiwa kwamba huyu mtoto katoka ndani analia kufika juu akaanguka mpaka kuzimia ikanibidi niende kwa mama anayeishi naye kumuhoji kwanini kampiga yule mtoto‘>>>Mjumbe
‘Mimi nafanya biashara huko Mbeya yule sio Msichana wa kazi nilikuwa naenda kwa Mama yake ndio tukawa kama ndugu huyu Msichana natoka naye Chombe ni mdogo wangu namfundisha kupika sasa leo kuna kitu kaniudhi nikamchapa, anatabia ukimchapa anajidondosha chini‘>>>Mama aliye mpiga mtoto
Full stori Play hapa chini usikilize…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE