Wakazi wa magomeni kota jijini Dar es salaam ambao waliamishwa na manispaa ya kinondoni na baadhi ya maeneo ya nyumba zilibomolewa na eneo hilo kuuzwa, wakazi hao walifungua kesi mahakamani kudai haki yao na wakawa wameshinda kesi hiyo.
Manispaa ilionekana kuchelewa kutekeleza maamuzi ya mahakama ya kuwarejesha waendelee kupanga na kuwaboreshea nyumba hizo, wakazi hao waliomba msaada kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi na aliwaahidi baada ya mwezi mmoja atatoa majibu baada ya yeye kufikisha suala hilo kwa Rais Magufuli.
Sasa leo August 01 2016 Waziri Lukuvi amekutana na wawakilishi wa wakazi hao ambapo amewapa majibu ya Rais Magufuli kwamba ameagiza kujengwa kwa nyumba 644 zenye bei nafuu na za kisasa magomeni kota na wakazi hao ambao walikuwa wanaishi hapo kuuziwa nyumba hizo kwa bei nafuu na kupewa kipaumbele kwa watakaopanga pia kwa wale watakaoamua kununua nyumba hizo watakuwa wanalipa taratibu.
Aidha Serikali imefuta mikataba yote ambayo Manispaa ya Kinondoni waliuza nakuingia mikataba hiyo kwenye maeneo ya magomeni kota.
Waziri Lukuvi pia ameelezeza kuwa Rais ametoa maagizo kuwa Nyumba zote nchini ambazo zilihamishwa kutoka NHC kwenda TAMISEMI 1991 serikali imeamua nyumba hizo zitasimamiwa na serikali kuu na wakazi hao wasihamishwe katika nyumba hizo. Wakazi hao wengi wao walikuwa ni watumishi wa serikali zamani na wamestaafu na wamekuwa wakiishi katika nyumba hizo.
ULIKOSA HII YA LOWASSA KUZUNGUMZIA KUHUSU UTENDAJI KAZI WA JPM? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI