Kwenye Leo Tena ya Clouds FM, Hekaheka ilikuwa inahusu tukio lililotokea Shinyanga ambapo mume amempiga mke wake mapanga hadi kumuua kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.
Wawili hao wamekuwa na tabia ya kugombana mara kwa mara ambapo ilikuwa inafikia wakati mwanamke huyo anarudi kwao, halafu mwanaume huyo anakwenda kumbeleza wanarudiana.
Mama wa marehemu amesema mwanaume huyo na mke wake Regina walikuwa na ugomvi uliosababisha Regina akarudi nyumbani, baadaye mume wake akaja kumuomba radhi, akakataa lakini baada ya mama wa mwanamke huyo kutoka alikuta wameondoka pamoja pasipo kujua namna ambavyo mwanamke alishawishika kurudi nyumbani na mume wake ambako mauti yalimkuta.
Jirani wa mwanamke huyo amesema alipokuwa anarudi kutoka kwenye shughuli zake alipata taarifa kuwa kuna mtu kauawa, na baada ya kwenda alikuta mwili wa Regina ukiwa chini na majeraha yanayoonesha kifo hicho kilitokana na kupigwa na kitu kizito sehemu za kichwani.
Unaweza kubonyeza play hapa kuisikiliza Hekaheka hiyo.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook