Mbunge wa Kawe Halima Mdee alishikiliwa na Polisi kwa siku tano ambapo jana July 10, 2017 alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka moja la kumkashifu Rais.
Halima Mdee alisomewa kosa hilo na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ambapo alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo July 3, 2017 akiwa Makao Makuu ya CHADEMA Dar es salaam ambapo baadae aliachiwa kwa dhamana.
Leo July 11 Halima Mdee ameingia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na kuandika kwa mara ya kwanza toka aachiwe kwa dhamana, maneno aliyoyaandika ni haya >>> “Kwa heshima KUBWA niwashukuru sana wote mliopaza sauti zenu kutaka haki itendeke kwangu na kwa watoto wetu wa kike! #Mapambano yanaendelea”
ULIPITWA? Halima Mdee yuko nje kwa dhamana, Freeman Mbowe kayaongea hapa… bonyeza play kwenye hii video hapa chini