Ripoti ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) inaonesha kuwa tatizo la fetma (obesity) yaani uzito ulipindukia duniani ni tatizo ambalo limeongezeka mara tatu zaidi ya jinsi lilivyokuwa mwaka 1975.
Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa tatizo hilo sio tu kwa mataifa yaliyoendelea kama Marekani, bali pia ni tatizo linalokua katika nchi zinazoendelea na kwamba matatizo ya uzito uliopitiliza yanahusishwa na sababu za vifo vingi duniani kuliko matatizo ya uzito wa chini (Underweight).
Matatizo ya uzito uliokithiri yanachangiwa na ongezeko la makampuni na biashara mpya za vyakula na vinywaji ambavyo vinakuwa vinauza bidhaa zenye viwango vya juu vya sukari na mafuta.
‘Kuna kikundi kimetumia mtandao wa Telegram kuhamasisha maandamano’-Polisi Makao Makuu