Mchezaji wa zamani wa vilabu vya AC Milan na FC Barcelona Christophe Dugarry ameonesha hasira za wazi wazi kwa mshambuliaji wa Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar kwa kitendo chake cha kutohudhuria game ya PSG dhidi ya AS Monaco.
Dugarry anaamini Neymar hajafanya sawa kitendo chake cha kutokwenda Ufaransa na kuendelea kubakia kwao Brazil wakati wa mchezo wa PSG dhidi ya AS Monaco uliyomalizika kwa PSG kupata ushindi wa magoli 7-1, ushindi huo ukawafanya watangazwe Mabingwa wa Ligi Kuu Ufaransa msimu wa 2017/2018.
“Kwa nini Neymar hakuwepo uwanjani kuangalia mechi yenye heshima ya kutangazwa Mabingwa? Neymar wanamuona kama kiongozi ameamua kutokuja kusherehekea na wachezaji wenzake? inakuwaje PSG wanakubaliana na kitendo hicho? anawachukuliaje wachezaji wenzake kwa tabia hiyo”>>> Dugarry
“Neymar anaidharau club na ameonesha ujeuri naamini kama angekuwa Barcelona basi angerudi bila shida yoyote, kama mimi ningekuwepo PSG basi ningepatwa na hasira sana kwa kitendo hicho”>>> Dugarry
Neymar alipewa ruhusa na PSG kwenda kujiuguza nyumbani kwao Brazil baada ya kupata jeraha la goti kutokana na kugundulika kuwa atakuwa nje ya uwanja hadi Kombe la dunia, imezoeleka hata kama mchezaji akiwa mgonjwa ni busara kujumuika na wenzake katika matukio muhimu ya timu kama kutangazwa Mabingwa.
ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1
https://youtu.be/-X6tg5a15HI