Kutoka mkoani Kagera leo March 5, 2018 imezinduliwa wiki ya elimu kwa mlipa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zoezi ambalo limefanywa katika viwanja vya Mayunga vilivyopo ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA Richard Kayombo akishirikiana na watumishi wa idara hiyo mkoani Kagera wameanza kusikiliza kero za walipa kodi ili kuona ni jinsi gani zinaweza kutatuliwa.
Aliyezindua zoezi hilo ni Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
“Ambae hajavaa kofia, kosa abebe yeye sio dereva” – Mwigulu
Mahakama ya Rufaa dhamana ya Rugemarila