Usiku wa March 21 2018 shirikisho la soka barani Afrika CAF lilichezesha droo ya game za mtoano wa michuano ya Kombe la shirikisho Afrika na Yanga ambao walikuwa wametolewa Club Bingwa Afrika wamepangwa kucheza dhidi ya Wolaitta Dicha F.C ya Ethiopia.
Mchezo wa kwanza wa Yanga dhidi ya Wolaitta Dicha F.C utachezwa Dar es Salaam kati ya April 6-8 na marudiano kati ya April 17-18, inawezekana huifahamu vizuri Wolaitta Dicha F.C kutokana na uchanga wake au ugeni wake katika michuano ya kimataifa.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wamekuwa na matumaini makubwa kufanya vizuri kwa timu yao dhidi ya Wolaitta Dicha F.C kutokana na timu hiyo kuwa ni ngeni katika michuano ya kimataifa na imeshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kutwaa taji la Ethiopian Cup ambao ni sawa na Kombe la ASFC la hapa.
Wolaitta Dicha F.C ni timu iliyoanzishwa mwaka 2009 na imepanda kucheza Ligi Kuu Ethiopia kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/2014 hivyo huu ni mwaka wake wa nne kucheza Ligi Kuu Ethiopia ambapo haijawahi kutwaa taji hilo zaidi ya Ethiopian Cup iliyotwaa kwa mara ya kwanza mwaka jana.
Club ya Wolaitta Dicha F.C imefuzu kucheza hatua hiyo kwa kuiondoa club Kongwe na yenye historia kubwa katika soka la Afrika Zamalek ya Misri kwa mikwaju ya penati 3-4, hiyo ni baada ya kucheza game zote mbili nyumbani na ugenini na kumalizika kwa kila mmoja kupata ushindi wa 2-1 akiwa nyumbani, wakati round ya kwanza ilipita kwa kuitoa Zimamoto ya Zanzibar, hivyo Yanga anapewa nafasi kwa kuwa na uzoefu wa game za kimataifa.
Unaweza kutazama walivyoitoa Zamalek kwa penati
https://youtu.be/B3PstyZwZog
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry