Moja kati ya stori kubwa zilizochukua headlines kwenye kiwanda cha Bongofleva ni pamoja na exclusive interview ya XXL ya Clouds FM na naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza iliyofanyika jana kwenye ofisi za BASATA.
XXL walifanya interview na naibu waziri Shonza na kuhoji masuala mbalimbali kuhusiana na sanaa ikiwemo maamuzi ya naibu waziri Shonza ya kufungia baadhi ya wasanii na nyimbo zao kwa madai ya ukosefu wa maadili kama Roma Mkatoliki aliyefungiwa miezi sita na Nay wa Mitego aliyepewa onyo na kuomba radhi.
Baada ya mahojiano hayo yaliyokuwa yamefanywa na kuhudhuriwa na viongozi wa BASATA, BAKITA huku Wakazi na Vanessa Mdee wakiwakilisha wasanii wenzao, kila mmoja amepokea majibu ya Naibu waziri kwa mtazamo tofauti.
Kwa upande wa Nay wa Mitego baada ya interview hiyo akaandika maneno haya katika ukurasa wake wa twitter “Kwa mahojiano ya leo mtakuwa mmeelewa tatizo ni nini? nauona mwisho wa huu muziki umekwamia hapa rasmi 2018, mkubwa atabaki kuwa mkubwa na mdogo ataendelea kuwa mdogo na tusivyo na umoja tunaenda walipokwenda ndugu zetu Bongo Movie”
Mbasha “Ninauwezo wa kwenda Mahakamani, sioni sababu ya Flora kuninyima mtoto”