Timu ya Real Madrid pamoja na kuripotiwa na kutopewa na nafasi na waandishi wengi wa habari za michezo nchini Hispania kuwa msimu uu haina nafasi ya kuwania taji la Ligi Kuu Hispania, mambo yamezidi kuwaendea kombo baada ya kucheza game yao ya ya LaLiga ugenini dhidi ya Espanyol na kujikuta wakipoteza mchezo wa tano wa LaLiga msimu huu.
Real Madrid inawezekana kumpumzisha Cristiano Ronaldo katika safari dhidi ya Espanyol inawezekana wakajutia kutokana na kukosekana kwa mchango wa staa huyo katika game dhidi ya Espanyol iliyomalizika kwa Espanyol kupata ushindi wa goli 1-0, goli ambalo limefungwa na Gerard Moreno katika dakika ya tatu za nyongeza kabla ya game kumalizika.
Ushindi huo sasa unaifanya Espanyol kufanikiwa kuviadhibu vilabu vyote vikubwa Hispania katika LaLiga vilivyocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid wote msimu huu wamepoteza kwa kufungwa goli 1-0, Espanyol wanafanikiwa kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Real Madrid baada ya miaka 11.
Katika michezo 23 ya LaLiga ambayo Espanyol alicheza na Real Madrid toka 2007, amefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee kwa goli 2-1, Espanyol wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani September October 20 2007, sare game tatu pekee na kuruhusu kufungwa game zote 19 zilizosalia, hivyo leo wanaweza kufanya sherehe kwa kuvunja rekodi hiyo.
VIDEO: Kocha msaidizi Simba baada ya kudaiwa kutopewa mkono na Ndemla