Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta siku ya Jumamosi ya November 4 2017 katika uwanja wao wa Luminus Arena alikuwa uwanjani kuitumikia Genk lakini kwa bahati mbaya hakumaliza game baada ya kuumia goti.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi Samatta alifanyiwa upasuaji wa goti lake la kulia na kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki sita hadi nane kwa ajili ya kuuguza hadi kupona jeraha lake, Samatta amerudi uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa siku 85 na baada ya kurudi aliongea haya.
“Nina furaha kurejea uwanjani unajua kama mchezaji wa mpira huwezi kufurahia kuwa nje ya uwanja lakini nina furaha nitafanya ninachotakiwa kufanya uwanjani majeruhi yameisha nilizungumza na Dr akaniambia sasa unaweza kucheza”>>> Samatta
“Kila mmoja anafahamu kuwa kesho ni mchezo wa nusu fainali na tunatakiwa kutwaa taji na kila mmoja anafahamu kuwa ni mchezo muhimu, siku zote napenda kufunga nitajaribu kufunga mara nyingi niwezavyo”>>> Samatta
VIDEO: Magoli ya John Bocco na Okwi yalivyoiua Majimaji FC leo