Kutokana na sakata la uuzwaji wa kampuni ya Tanga Cement kumekuwa na mijadala mingi juu ya uuzwaji wa asilimia 68.33 ya hisa za Tanga Cement PLC ambapo mijadala hii imeibua sintofahamu kwenye jamii kutokana na watu wengi kutoelewa juu ya mchakato mzima na faida itakayo patikana endapo kampuni ya Scancem Internationa Da itafanikiwa kununua hisa hizo.
Kutokana na wasiwasi pamoja na malalamiko kutoka kwa wazalishaji wengine wa simenti nchini juu ya uuzwaji kwa kampuni ya Tanga Cement ambako kutasababisha mwekezaji mmoja kutawala soko la simenti nchini na hii kumwezesha mzalishaji mmoja kumiliki asilimia zaidi ya 35 la soko la simenti nchini, hii taarifa si kweli.
Mmoja ya wafanyakazi wa kampuni ya Tanga cement ambae hakutaka jina lake litajwe ameeleza kuwa endapo mtu atajaribu kufanya utafiti rahisi tu ambao hauhitaji gharama kubwa na kuweza kujua idadi ya viwanda vya simenti nchini ambavyo vinazalisha kwa ukamilifu na vile ambavyo husaga simenti, atakutana na idadi kubwa ya viwanda hivyo.
“Viwanda hivi huzalisha zaidi ya kile ambacho nchi yetu inaweza kutumia. Kwa lugha nyingine tunaweza sema kuwa usambazaji wa bidhaa ni zaidi ya uhitaji wa sokoni. Hivyo hakuna namna ambavyo mzalishaji mmoja anaweza kutawala soko lililo na wazalishaji wengi,”
“Endapo ununuzi huu utafanikiwa, ni dhahiri kuwa kampuni ya Scancem Da, itatakiwa kurekebisha hali ya kampuni hasa upande wa kiufundi, na kuhakikisha kiwanda kinaendeshwa vizuri kwa faida ambayo watanzania wote watanufaika kutokana na upatikanaji kwa bidhaa muda wote huku Serikali ikiendelea kujipatia mapato ambayo Tanga Cement kwa kipindi kirefu ilishindwa kulipa kwa muda mrefu,”.
Tanga Cement itabadilika kutoka kampuni iliyokuwa inapata hasara na kuwa kampuni inayotengeneza faida.
Kwa ujumla ununuzi huu utaleta mfumo mpya wa undeshaji wa Viwanda vya simenti nchini kutoka na na mabadiliko haya. Labda wazalishaji wengine wana wasiwasi kutokana na changamoto ya kiteknolojia ambapo itawalazimu kubadilika kiteknolojia ili kuweza kuendana na ushindani.
Uuzwaji wa Tanga Cement unaungwa mkono na wadau wote wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wote wa Tanga Cement.