Mbunge wa Kahama Mjini Jumanne Kishimba leo Bungeni Dodoma amehoji kwanini Serikali inakataa mabati kuanzia geji 33 mpaka 40?
“Wataalamu wetu asilimia 90 wanajua kusoma na kuandika sio maarifa, hapa tunapolia mabati Serikali inakataa kuanzia geji 33 mpaka 40 kwa nini? na imepiga marufuku nyumba za nyasi na za tembe mfano wewe unashida nyumbani kwako huna hela ya kula ugali mweupe si unasaga dona na hii elimu ya kwenu ndio ilitutoa sisi kwenye nyasi ikatupeleka kwenye bati nyie mlikuja mkatuambia nyumba za nyasi ni mbaya anzeni kutumia mabati, leo mabasi yamepanda mnatuwekea sheria tena tusitumie ya geji 40 kwa sababu gani?”-amehoji Mbunge Kishimba akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.