Mchezaji mpya wa Manchester United aliyesajiliwa kwa pauni milioni 72, Rasmus Hojlund, hatacheza mechi yake ya kwanza kesho dhidi ya Nottingham Forest.
Hata hivyo, kocha wake Erik ten Hag alithibitisha kuwa hatakuwepo kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi.
“Sio kwa kesho.
Leo kwa mara ya kwanza aliingia kwenye mazoezi ya timu hivyo wiki ijayo natarajia atafanya wiki nzima. Yuko karibu sana kukinoa kikosi,” aliwaambia waandishi wa habari.