Vifaa vya kupima vimegundua visa 24 vya Hepatitis A miongoni mwa wakazi wa Gaza, anasema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus ambaye aliongeza kuwa pia anafahamu kuhusu visa elfu kadhaa vya homa ya manjano katika eneo lililozingirwa.
Hepatitis A, kuvimba kwa ini, mara kwa mara inaweza kusababisha ugonjwa mbaya.
“Hali za maisha zisizo za kibinadamu – bila maji yoyote safi, vyoo safi na uwezekano wa kuweka mazingira safi – itawezesha Hepatitis A kuenea zaidi na kuonyesha jinsi mazingira yalivyo hatari kwa kuenea kwa magonjwa,” aliandika kwenye X.
Tazama pia..