Makumi ya wanaharakati mashuhuri huko Hong-Kong wamehukumiwa hivi hadi miaka 10 jela ikiwa ni miongoni mwa kesi kubwa zaidi inayowahusisha na vitendo vya kuhatarisha usalama wa taifa.
Washtakiwa hao wapatao 47 na waliofunguliwa mashitaka mwaka 2021, walikuwa wakikabiliwa na kifungo cha maisha jela chini ya sheria kali iliyowekwa na Beijing na iliyokandamiza vuguvugu la kuunga mkono demokrasia ambalo lilijizolea umaarufu mkubwa.
Washtakiwa 45 aidha walikiri shitaka la kula njama ya kufanya uasi au walipatikana na hatia na majaji watatu walioidhinishwa na serikali kuhusu mipango ya wanaharakati hao ya kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi usio rasmi ambao ungeidhoofisha mamlaka ya serikali katika mji huo wa Hong-Kong na kusababisha mgogoro wa kikatiba.
Hata hivyo washtakiwa wawili kati ya hao wameachiwa huru. Waangalizi wanasema kesi hiyo inaonyesha ni kiasi gani mamlaka inavyokandamiza upinzani na vyombo vya habari kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali ya mwaka 2019.