Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma, imeanza kufanya upasuaji mkubwa wa moyo, ambapo watoto wanne wameshafanyiwa upasuaji huo, huku wengine wanane wakipatiwa matibabu ya moyo kwa kutumia maabara maalum, ili kuziba matundu na kupanua mshipa mkubwa wa moyo.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, kufuatia uchunguzi waliofanya kwa Watoto 123 na asilimia 90 kubainika kuwa na matatizo ya moyo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika alisema.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Moyo kutoka For Heart and Souls nchini Marekani Dkt. Kirk Milhon, ameweka wazi lengo lao ni kuwafundisha madaktari wa kitanzania jinsi ya kuendesha upasuaji huo mkubwa, na wameanza na kesi ndogo za moyo na wataenda hatua kwa hatua hadi kutibu magonjwa makubwa ya moyo.
Kufuatia operesheni moja kugharimu kati ya shilingi milioni 20 hadi 30 baada ya serikali kuweka ruzuku, huku wanaotibiwa kwa sasa wakitibiwa bure baada ya wadau kulipia gharama hizo, Katibu Mkuu Mtendaji wa The One New Heart Tanzania. Margreth Elias akawa na ombi kwa serikali, huku mmoja wa wazazi mwenye mtoto aliyefanyiwa upasuaji na mkazi wa Ulanga Morogoro Bw. Rayson Maji akiwashukuru wadau, kwa kuwa sasa hana bima baada ya kustaafu kwenye utumishi wa umma.
Hii inakuwa ni hospitali ya pili nchini kufanya upasuaji mkubwa wa moyo, baada ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKNCI), na hivyo kuanza kupunguza msongamano katika hospitali hiyo.