Hospitali ya Mkoa wa Jalalabad nchini Afghanistan inakabiliana na janga la njaa inayoshika hatamu, huku Watoto wakipambana na matatizo makubwa ya lishe.
Amina, mama mwenye huzuni, amepoteza Watoto wake sita kutokana na njaa kali, na sasa anakabiliwa na hali ngumu kwa Mtoto wake wa miezi saba, Bibi Hajira, ambaye anakabiliwa na utapiamlo mkali.
Watoto 18 wanalala katika vitanda saba kwenye Wodi hii, ambapo wengi wanashindwa hata kusogea kutokana na udhaifu wao, Magonjwa mengine yanayoweza kuzuiliwa pia yanachangia kuongezeka kwa Vifo vya Watoto, kama vile Pneumonia kali inayomshikilia Umrah, Mtoto wa miezi sita.
Ingawa Hospitali inajitahidi kwa kadri ya uwezo wake, ukosefu wa Vifaa na Dawa unakwamisha jitihada za kuokoa maisha zaidi, Maisha ya Watoto wengine wanakumbwa na hali ngumu sana kutokana na ukosefu wa Fedha, huku Familia zikikabiliwa na hali ya umaskini mkubwa na mgogoro wa kisiasa unaoathiri misaada ya Kimataifa.
Kutokana na hali hii, UNICEF inasema kwamba Watoto wanakabiliwa na madhara ya muda mrefu kutokana na Utapiamlo na ukosefu wa matibabu, hata hivyo, jitihada za haraka zinaweza kusaidia kuokoa maisha ya Watoto na aina hii ya msaada inahitaji kuungwa mkono zaidi ili kuboresha hali ya afya na lishe ya Watoto nchini Afghanistan.