Hamas imetoa taarifa ikisema hospitali zote za Gaza zimekosa mafuta.
Kundi hilo la wapiganaji linatoa wito wa kuwepo kwa korido ya kudumu katika eneo hilo ili kuepusha “janga la kibinadamu”.
“Mzingiro unaoendelea ulilemaza hali ya kibinadamu na kusababisha uhaba mkubwa wa chakula na dawa. Bila kusahau kwamba hospitali zote za Ukanda wa Gaza zimekosa mafuta,” ilisema.
Hamas ilikosoa kiwango kidogo cha misaada inayoruhusiwa kuingia Gaza na kuzitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu, pamoja na Umoja wa Mataifa, “kuongeza juhudi” za kufungua ukanda wa kibinadamu.
“Ukanda wa Gaza haujafanyiwa chochote isipokuwa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambao ukiendelea, utakuwa ni aibu kabisa kwa ubinadamu,” ilisoma taarifa hiyo.