“Siku mbili zilizopita tuligundua kunguni na inatisha,” anasema Max Malka, mmiliki wa Hoteli ya Montlhery Paris Sud, kilomita 15 kusini mwa Paris.
Hujui ikiwa wanatembea kati ya vyumba, alisema, na unaweza kushtakiwa ikiwa mgeni ataumwa vibaya.
Yake ni mojawapo ya makampuni mengi yanayotafuta suluhu huku kukiwa na ongezeko la milipuko wa kunguni iliyoripotiwa nchini Ufaransa na Uingereza.
Na makampuni yanageukia teknolojia – ya zamani na mpya – ili kupata ufumbuzi mapema, ambayo ni muhimu kukomesha kuenea.
Kuna wasiwasi unaoongezeka wa umma kuhusu wadudu hao, huku hoteli, kampuni za usafiri na serikali za mitaa zikikabiliwa na maswali kuhusu suala hilo.
Kampuni ya kudhibiti wadudu ya Rentokil ilisema iliona kuongezeka kwa 65% kwa visa vya kunguni nchini Uingereza katika robo ya pili ya 2023, ikilinganishwa na mwaka mmoja mapema.
Na Baraza la Luton lilitoa mwongozo kwa wakaazi wa eneo hilo wiki hii juu ya jinsi ya kushughulikia milipuko, baada ya kushughulikia “idadi kubwa” ya simu kuhusu kunguni.
Bw Malka anadokeza kuwa hoteli za Paris zinaweza kutarajia kupata kesi mara moja kwa mwaka. Kawaida, kunguni hao huletwa na wageni wanaposafiri katika msimu wa kiangazi.