Watu watatu wamefariki dunia wakiwiwemo watoto wawili wa familia moja ambao ni Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwazoka kuuawa kikatili baada ya kukatwa katwa na mapanga na Mfanyakazi wa kazi wa ndani wa kiume aliyetambulika kwa jina la Yasin Abdalah mwenye umri wa miaka 35 kisha na yeye kuuliwa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Mwakyo Nyigesa amesema tukilo hilo limetokea jana majira ya saa moja usiku katika kitongoji cha Kivungwi Kazoka Kata ya Vingwaza kilichopo Wilayani Bagamoyo.