Kutoka nchini Syria taarifa ni kwamba watu 38 wameuawa kwa bomu lililolipuliwa kwenye eneo la soko katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus siku ya jana March 20, 2018.
Tukio hili linaelezwa kuwa sehemu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo kwa sasa serikali ya nchi hiyo inataka kuukomboa mji wa Ghouta Mashariki ambao unashikiliwa na kikundi cha waasi.
Inasemekana kuwa ndege aina ya rocket zinazomilikiwa na waasi hao ndizo zilizorusha na kulipua eneo hilo la soko na kusababisha maafa hayo huku 20 wengine wakijeruhiwa.
Jitihada hizo za serikali ya Syria kuchukua eneo hilo la Ghouta Mashariki ambapo ni makazi kwa watu takribani 400,000 kutoka kwa waasi, zimesababisha vifo vya 1,400 huku watu 45,000 wakikimbia makazi yao.
Kauli ya Waziri Jafo baada ya Kuwaita wakuu wote wa mikoa