Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afri Transport, raia wa Tanzania, Mohammed Ameenullah Kashmiri (82) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kuajiri raia wa Uingereza kinyume na sheria.
Raia hao wa Uingereza ambao nao wamefikiswa Mahakamani ni Mohammed Mobeenullah Kashmiri (72) na Saleem Kashmiri (50). Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Gerald Maridai amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka tisa.
Katika kesi hiyo ya jinai namba 17 ya 2018, Mohamed Ameenullah Kashmir anakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kutoa taarifa za uongo ili kuwapatia vibali vya kufanyia kazi raia hao wa Uingereza.
Inadaiwa October 25, 201 7 Mohamed Ameenullah Kashmiri alitoa taarifa za uongo ili kuwapatia vibali vya kuishi nchini raia hao, pia aliwaajiri raia hao wa Uingereza wakati hawana vibali vya kufanya kazi nchini.
Hakimu Mwambapa alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh 20 milioni. Pia wasalimishe hati zao za kusafiria mahakamani na wasisafiri nje ya nchi bila ya kibali cha Mahakama.
Kesi imeahirishwa hadi February 19, 2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
‘Afya ya Rugemarila, Seth zinatia mashaka’ Wakili
Kilichozungumzwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Naibu wake na Majaji baada ya kuapishwa na JPM