September 6 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib amekutana na hii iliyotokea Tegeta, Dar es salaam ambapo baba mdogo kampa mimba mtoto wake millardayo.com imekurekodia full stori kutoka kwenye Hekaheka ya leo.
Imeelezwa kwamba binti wa miaka 16 ambaye alikuja kama msichana wa kazi za nyumbani baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi 8 muajiri wake akagundua kuwa binti ni mjamzito na alipomhoji akasema ujauzito ni wa baba yake mdogo ambaye ni mume wa mama yake mdogo.
Binti alifanikiwa kujifungua lakini bahati mbaya mtoto alifariki na ikadaiwa mtoto asizikwe mpaka baba wa mtoto ajitokeze, baba huyo hakuwa tayari kujitokeza huku akisisitiza kuwa mke wake asiambiwe chochote.
Kupata full story bonyeza play hapa chini
ULIKOSA KUTAZAMA HII YA SILAHA ZA MAJAMBAZI ZILIZOKAMATWA NA JESHI LA POLISI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI