Uenda ukosefu wa ajira ukapungua kwa vijana wa Kitanzania baada ya kampuni mbalimbali kutoka nchini Canada kukutana na serikali ya Tanzania ili kutafuta mbinu za kuwainua vijana kupitia uchimbaji madini na gesi.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo February 1, 2018 Kamishna wa Madini Tanzania, Prof. Shukran Manya amesema lengo la kampuni hizo za Canada kukutana na serikali ya Tanzania na wadau ni kujadili maendeleo katika sekta za madini na gesi.
Prof. Manya amesema katika mkutano huo wanatafuta ni jinsi gani wanavyoweza kuwasaidia vijana wa Kitanzania kupata maendeleo kupitia sekta hizo.
Pia amesema kampuni hizo zinazungumzia jinsi ya kufuata sheria na kanuni za nchi katika sekta ya madini na gesi.
Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji wakubwa wa madini nchini, Ami Mpungwe amesema changamoto kubwa inayokabili sekta ya madini ni vijana kutokuwa na taaluma ya kutosha katika sekta hiyo.
Kitaalamu madhara ya kuzuia chafya