Ikiwa ni siku chache tangu taarifa ya mzee ambaye alidaiwa kubuni na kuchora Nembo ya Taifa kuripotiwa na Serikali kuamua kumpatia msaada wa matibabu, familia moja imeibuka na kudai mzee huyo anayetajwa kuhusika kubuni siyo, bali ni mzee wao na ameshafariki.
Serikali kupitia Wizara ya Afya iliamua kumsaidia kimatibabu mzee Francis Maigemaarufu kama ‘Ngosha’ ambaye alilazwa Hospitali ya Amana na kuamua kumhamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo baada ya tukio hilo familia nyingine imeibuka na kudai kuwa mzee wao ambaye sasa ni marehemu ndiye mchoraji wa Nembo hiyo.
Ayo TV na millardayo.com zimekutana na familia hiyo ambayo imeamua kufunguka na kuelezea kila kitu ukiwepo ushahidi wa mzee wao kuchora Nembo hiyo.
“Ushahidi ambao tunao ni wale watu wa rika lake ndiyo walikuwa wanashuhudia kwamba yeye ndiye aliyechora.” – Yehoshaphat Jeremiah Kabati (Mtoto wa tatu wa anayedaiwa kuchora Nembo ya Taifa)
ULIPITWA??? Serikali baada ya taarifa ya Mbunifu wa Nembo ya Taifa…