Bila shaka umewahi kusikia watu mbalimbali wakifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kupandikiziwa viungo mbalimbali vya mwili kama figo, moyo, macho na vinginevyo.
Kwa msichana Paigey Cakey imekuwa ni tofauti kidogo ambapo yeye amefanyiwa upasuaji wa kupandikizwa nywele baada ya kuugua ugonjwa ambao ulifanya nywele zake zianze kunyofoka kidogo kidogo.
Paigey ambaye ni Mwanamuziki wa London ameeleza kuwa aligundua anatatizo hilo la nywele kuanguka akiwa na miaka 18 jambo lililomfanya atumie mascara kuchora maeneo yasiyo na nywele ili tu asionekana kuwa na kipara kwenye baadhi ya maeneo ya kichwa chake.
Binti huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama traction alopecia ambao unatokana na kutengeneza nywele au kuvaa mawigi yanayobana sana kichwa, au kusuka nywele zilizokaza sana jambo alilokiri kuwa alikuwa akilifanya sana akiwa bado chuo.
November 2018, alifanyiwa upasuaji wa kupandikizwa nywele na ameeleza kuwa tatizo hilo limemfanya aone nadharia ya urembo au uzuri kwa mtazamo mpya
Mchungaji awalazimisha Waumini kubusu na kulamba viatu vyake