Baada ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF) Malangwe Ally Mchungahela kutangaza mchakato wa uchaguzi mkuu wa Yanga, baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa Yanga na wanachama wa club hiyo wadaiwa kuwa watakaa kikao kesho kupinga mchakato huo.
Mashabiki na baadhi ya wanachama wa Yanga wanadaiwa kutokuwa tayari kukubali kufanya uchaguzi mkuu wa kumchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa club hiyo, kwani wengi wanaamini kuwa mwenyekiti wao Yussuf Manji bado yupo na wanamtambua kama kawaida ila Manji amekaa kimya mwenyewe hajatoa tamko lolote.
“Mchakato wa uchaguzi wa Yanga ulishaanza tayari tangu tulipoutangaza tarehe tano na fomu zilikuwa zianze kuchukuliwa tarehe nane lakini tarehe nane hatukuweza kwa sababu tulikuwa na kikao na wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanga na tukakubaliana baadhi ya masuala fomu zikatoka tarehe 9″>>>Malangwe Ally
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19