Rais wa Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi amewasili mchana wa leo December 14, 2017 nchini kwenye ziara yake ya siku moja ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli Mjini Dodoma.
Ujio wa Rais huyu umelenga kuimarisha na kukuza uhusiano baina ya nchi hizi mbili na kuzungumza namna zitakavyo badilishana uzoefu kuhusu ugunduzi mkubwa wa gesi na mafuta uliofanikiwa katika nchi hizi, masuala ya ulinzi na usalama na uimarishaji wa miundombinu ya usafiri.
“Nafurahi kuwa Mhe. Rais Nyusi pia amesema Msumbiji itatoa kibali kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kufanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Msumbiji haraka iwezekanavyo, ili kurahisisha usafiri kati yetu” – Rais Magufuli.
Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala